Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa inafanya uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowahusu wafanyabiashara wa sukari nchini kwa kuficha bidhaa hiyo ili kusababisha upungufu katika soko na hivyo kuleta usumbufu kwa jamii ya watanzania wanaohitaji bidhaa hiyo kwa matumizi jambo ambalo limesababisha kupanda kwa bei ya sukari
.
TAKUKURU imeanza uchunguzi dhidi ya Tuhuma hizi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na tayari twametembelea Maghala ya mfanyabiasha Haruni Daudi Zacharia ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Al-Naeem yaliyoko Mbagala na Tabata ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa nchini wa sukari na anayetuhumiwa kuficha bidhaa hii.
Mnamo tarehe 05 Mei, 2016 timu ya uchunguzi ilitembelea maghala ya Tabata na kubaini uwepo wa sukari yenye jumla ya tani 4,579.2 iliyonunuliwa toka Kiwanda cha Kilombero Sugar Company.
Kwa mujibu wa TAKUKURU, uchunguzi ulibaini kuwepo kwa njama za dhati za kutouza sukari kulikofanywa na mfanyabiashara huyo kwani hata sehemu ya Maghala ilipo sukari hapakuwepo dalili za upakiaji wa sukari na baada ya kufika Kitumbini maafisa walibaini uwepo wa wananchi wengi waliokuwa wakihitaji bidhaa hiyo.
Uchunguzi uliofanyiwa na TAKUKURU kwa kushirikiana na Polisi umebaini kuwepo kwa mikakati ya dhati iliyokuwa ikifanywa kwa kununua sukari yote toka viwanda vya ndani na kisha kuihifadhi na kuuza bidhaa hiyo kidogo kidogo kwa wastani wa tani 250 kwa siku .
Kuficha bidhaa ni kosa la uhujumu uchumi na ni kinyume na Aya ya 3 Jedwali la kwanza Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 [Chapisho la Mwaka 2002].
TAKUKURU inatoa wito kwa wafanyabiashara wote wa sukari kuacha vitendo vya kuficha sukari na vyombo vya uchunguzi vinafuatilia kote nchini na yeyote atakayebainika kufanya hujuma hizo atakabiliwa na mkondo wa Sher
No comments:
Post a Comment