Wednesday 25 August 2021

HAJI MANARA ATOA NENO KUHUSU JEZI MPYA YA YANGA.


KLABU ya Yanga leo Agosti 25, 2021 wamefanya uzinduzi wa jezi mpya za msimu wa 2021/22 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo fupi ni Haji Manara alikuwa mshika kipaza na kuongoza shughuli nzima ambayo ilihudhuriwa pia na Waandishi wa Habari.

Manara amesema kuwa ni uzi bora kuwahi kutokea ndani ya Afrika Mashariki na kuwaomba mashabiki waweze kuununua uzi huo kwa wingi bila kusahau kujitokeza kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi, Agosti 29, Uwanja wa Mkapa

No comments:

Post a Comment