Lwandamina ameondoka leo kurejea kwao Zambia na awali ilielezwa ni matatizo ya kifamilia, lakini yeye mwenye amesema kwamba amepata msiba mkubwa.
"Nimepata msiba mkubwa, nimempoteza baba yangu mzazi siku chache zilizopita. Sasa narejea nyumbani kwa ajili ya mazishi," alisema.
Kocha huyo mtaratibu amesema atarejea na kujiunga na kikosi chake mara tu atakapomaliza suala hilo la mazishi ya mzazi wake.
No comments:
Post a Comment