Thursday, 16 June 2016

Jukwaa la katiba Tanzania latoa kauli hii kwa Rais Magufuli juu ya Katiba.

dPLy26cfybruhXPIHvnPmjl72eJkfbmt4t8yenImKBVvK0kTmF0xjctABnaLJIm9
Jukwaa la katiba Tanzania (JUKATA) limemtaka Rais Dk John Pombe Magufuli kulitangazaa taifa tarehe ya kurejea kwenye mchakato wa katiba mpya na namna ya kukamilisha hatua iliyobaki kuelekea kura ya maoni.

Hatua hizo ni pamoja na kuitishwa kwa mkutano mkuu wa kitaifa wa katiba ambao utalazimika kupitia maudhui ya katiba inayopendekezwa ikilinganishwa na rasilimali ya tume ya mabadiliko ya katiba kwa lengo la kuainisha malalamiko yanayotolewa na wananchi .

Mwenyekiti wa bodi ya Jukwaa la katiba Tanzania Deus Kibanda amewaambia waandishi wa habari wakati anatoa mapendekezo kwa serikali juu ya sheria zilizopitwa na wakati  ya mwaka 2011 na ile ya kura ya maoni ya 2013 ambayo imeendelea kutumika hadi leo bila ya kufanyiwa  marekebisho.

Aidha Bw. KIbamba ameeleza kuwa sababu kuu ya kufufua upya mjadala kuhusu mchakato wa katiba ni kutokana na uzoefu wa JUKATA kwenye michakato ya katiba duniani na hasa barani Afrika ambako viongozi wapya wanapoingia madarakani huwa na tabia ya kupuuza maswala yaliyoanzishwa na watangulizi wao na kujielekeza katika masuala wanayoamini yanafaa kwa kwa wananchi na utawala wao.

No comments:

Post a Comment