Wednesday 17 August 2016

Mh.Paul Makonda atoa agizo hili kwa wakuu wa wilaya kuhusu wamachinga wa Msimbazi na Mtaa wa Kongo.


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.Paul Makonda,leo ametoa agizo na kuwapa "ultimatum"(kauli ya mwisho) viongozi na wakuu wa Wilaya za Dar es salaam kuhakikisha ndani ya wiki moja,wamachinga wote waliovamia maeneo yasiyoruhusiwa kama Msimbazi na mtaa wa Kongo kuondolewa haraka na kupelekwa ktk maeneo maalumu waliyopangiwa na Jiji.


Akiongea na Waandishi wa Habari ofisini kwake, Makonda anasema "tamko la Rais" alilolitoa mkoa wa Mwanza ktk viwanja vya Furahisha ni kama limetafsiriwa vibaya,kwani sasa Machinga wamevamia jiji la Dsm katika yale maeneo waliyokuwa wanaondolewa ili kuepusha msongamano.

Makonda ametoa mfano wa mtaa wa Msimbazi ambapo Wamachinga kwa sasa wamepanga bidhaa zao sehemu za watembea kwa miguu na hivyo kuzua msongamano usio na sababu huku vibaka na wezi wengine wakitumia maongamano huo kutekeleza vitendo vyao vya uhalifu.

Mh.Makonda anasema ukienda mtaa wa Kongo ndio haupitiki kabisa,si kwa gari wala kwa pikipiki,na hata watu wanaoenda kununua mahitaji yao wanapata shida ya msongamano sababu wamachinga wamelaza na kupanga bidhaa zao chini ambapo ni sehemu ya watembea kwa miguu,hivyo kusababisha msongamano pia wa magari na ajali zinazoweza kuzuilika.

Eneo la Msimbazi kituo cha Polisi na karibu na Bank ya Posta,Wafanyabiashara hao wamepanga bidhaa mpaka kwenye tuta linalotenganisha barabara za magari ya kawaida na mabasi ya mwendo kasi,hivyo kuzua hofu ya watu kugongwa au kuweka mazingira ya ajali.Eneo hilo katikati ya hizo barabara si tu hairuhusiwi machinga kupanga biashara zao,bali hata katika matumizi ya kila siku hata watu tu watembea kwa miguu hawaruhusiwi kutembea.

Hivyo kuondoa hali hiyo,agizo limetolewa kwa wakuu wa mikoa na viongozi wa Jiji,kuhakikisha machinga wameondolewa haraka na kupelekwa walikopangiwa,kwani hata rais hakusema wakapange vitu barabarani bali katika yale maeneo ambayo yameruhusiwa.



USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment