VIJANA watano wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumdhalilisha Rais Dk. John Magufuli na Jeshi la Polisi kutokana na mauaji ya askari polisi wanne waliouawa na majambazi katika eneo la Mbande na Vikindu, Dar es Salaam hivi karibuni.
Washtakiwa hao walifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya mahakimu watano tofauti na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Salum Mohammed.
Walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Emmilius Mchauru, Huruma Shahidi, Margareth Bankika, Dk. Yohana Yongolo na Respicius Mwijage.
Akisomewa mashtaka, mshtakiwa Dennis Mtegwa anadaiwa Agosti 24, mwaka huu eneo la Ubungo External kupitia mtandao wa WhatsApp, aliweka maoni katika group linaloitwa Dsm 11 4u Movement, akisema
‘JPM sijui anawaza nini kichwani… hata samahani hajui au nilikosea hajui’, ‘nchi imefika hapa kwa sababu ya mtu mmoja aliyeamua kujilipua ufahamu wake’, ‘sijaona tatizo kwa hilo, ila kwa huyu bwana misimamo ambaye amesema msinijaribu na ilhali kajaribiwa na ubwabwa wa jubilee kusema yote’.

‘Siasa si chuki wala upinzani si uadui, ajifunze kushindana kwa hoja sio mitutu ya bunduki na mazoezi yasiyo na kichwa wala miguu ya polisi’.
Mshtakiwa Suleiman Saidi anadaiwa Agosti 25, mwaka huu maeneo ya Kigogo, kwa kutumia mtandao wa Facebook, aliandika
‘Safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au’.
‘Safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au’.
Katika kesi nyingine, mshtakiwa Juma Mtatuu akiwa eneo la Ocean Road, Agosti 24, mwaka huu anadaiwa kuwa alituma ujumbe katika Facebook akisema
‘Huyu hata akifa ataenda peponi, na kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala, mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana kule Kahama, tarehe moja naelekea Kahama kwa Ukuta, mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta, kifo kipo tuu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha’
USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA
ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE
No comments:
Post a Comment