Tuesday 29 November 2016

Chama cha Kikomunisti cha china cha wasili Tanzania kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa CCM.

UJUMBE wa watu sita kutoka Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umewasili nchini kwa ziara ya siku saba kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida alisema ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa chama hicho, Jia Bo.

Madabida alisema ziara ya ujumbe huo hapa nchini ni kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na China ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa na kiongozi wa Taifa hilo Hayati Mao  Tse-Tung.



Alisema ujumbe huo ambao utatembelea Wilaya ya Temeke na Zanzibar umewasili nchini kufuatia ziara ya baadhi ya makada wa CCM walipokwenda nchini China ambapo walijifunza mambo mbalimbali ambayo ujumbe huo utapenda kujua kama wameyafanyia kazi.

Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Pindi Chana alisema ujio wa viongozi wa chama hicho kutoka China ni matunda ya ushirikiano wa Tanzania na nchi mbalimbali duniani.

" Ujio wa wenzetu hawa kutoka China ni matunda ya ushirikiano kati yetu na nchi nyingine kama Zimbabwe, Afrika Kusini, Angola, Cuba,  Ulaya hasa katika siasa za kijamaa" alisema Chana.

Alisema wenzetu wa China wapo karibu bilioni moja na wamepiga hatua katika maeneo mbalimbali hivyo ujio wao hapa nchini ni fursa kwao kujifunza mambo yetu na sisi kujifunza kwao kutokana na hatua ya kiuchumi waliyonayo.


USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE




                                SUBSCRIBE ON YOUTUBE 
                                          
                                               TIKISA TV

No comments:

Post a Comment