Tuesday, 25 July 2017

Kelvin Yondani aanza mazoezi Rasmi.

Image result for Kelvin Yondani
Baada ya kukamilisha shughuli zake za kufunga ndoa, beki kisiki wa Yanga, Kelvin Yondani ameanza mazoezi ya taratibu.

Yondani ameanza mazoezi taratibu kuanzia jana na leo anatarajia kuungana na wenzake katika mazoezi ya pamoja.

Beki huyo ambaye amekuwa tegemeo la Yanga katika safu ya ulinzi, amejiunga na timu hiyo jana baada ya kukamilisha shughuli zake za kufunga ndoa.

No comments:

Post a Comment