Thursday, 21 September 2017

Kim Jong-un aifananisha hotuba ya Trump sawa na mbwa anayebweka.

Image result for Kim Jong-un
Mwanadiplomasia wa cheo cha juu wa Korea Kaskazini ameifananisha hotuba ya Trump kwa Umoja wa Mataifa na kibweko cha mbwa.

Akihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano, Bw Trumo alisema kuwa ataiharibu Korea Kaskazini ikiwa itakuwa tisho kwa Marekani na washirika wake.
Matamshi ya waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Ri Yong-ho, ndiyo ya kwanza rasmi ya Korea Kaskazini tangu hotuba ya Trump.
Makombora ya Korea Kaskazini
Makombora ya Korea Kaskazini
Korea Kaskazini imendelea na mpango wake wa nyuklia na kukiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa.
"Ikiwa Bw Trump anafikiri kuwa atatuletea hofu kwa sauti ya mbwa anayebweka basi hiyo kwake ni ndoto."
Akizungumza kuhusu kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jon-un, Bw Trump aliuambia Umoja wa mataifa kuwa Bwana Kim ako katika mikakati ya kujitia kitanzi.
Wanajeshi wa Marekani walio Korea Kusini
Image captionWanajeshi wa Marekani walio Korea Kusini
Bwana Ri anatarajiwa kutoa hotuba yake kwa Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa.
Wataalamu wanasema kuwa Korea Kaskazni imaharakisha mipango yake ya kuunda makombora ya masafa marefu na mipango yote ya nyuklia.
Tarehe tatu Septemba Korea Kaskazini ilitangaza kuwa imefanya jaribio lake la sita la nyuklia.

No comments:

Post a Comment