Chini
ya Kocha Jupp Heynckes aliyerejea baada ya kutimuliwa kwa Carlo
Ancelotti, Bayern Munich imeanza kwa kuitwanga Freiburg kwa mabao 5-0.
Katika mechi hiyo ya Bundelisga, Bayern ingeweza kushinda kwa mabao mengi zaidi.
Mabao
ya Kingsley Coman, Thiago, Robert Lewandowski, Joshua Kimmich na moja
la kujifunga imeifanya Bayern irejee katika mwendo wake uliozoeleka.
No comments:
Post a Comment