Niyonzima amezungumza na kusema kiwango chake hakijawa kama anavyotaka.
"Kweli sijafikia kama ninavyotaka, ndiyo maana nimeamua kufanya mazoezi ya ziada.
"Nafanya hivyo ili kuwa katika kiwango ninachotaka. Hii inatokana na kwamba sikupata muda mzuri wa mazoezi mwanzoni mwa msimu," alisema.
Niyonzima alichelewa kujiunga na kikosi cha Simba na alishindwa kujiunga nacho wakati kikiwa kambini nchini Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya.
Wakati huo ndiyo alikuwa amejiunga na Simba akitokea Yanga lakini alibaki nchini kwao Rwanda kwa ruhusa ya uongozi wa Simba kwa kuwa alikuwa akisomea ukocha.
No comments:
Post a Comment