Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku anafaa kuheshimiwa na mashabiki na hafai kukosolewa kulingana na mkufunzi wake Jose Mourinho.
Lukaku aliyesajiliwa kutoka Everton kwa dau la £75m alifunga mabao 11 katika mechi zake 10 za kwanza lakini hajafunga hata bao moja katika mechi zake tano za mwisho.
''Kile anachoifanyia timu hii ni kazi nzuri na kucheza soka kama mshambuliaji sio kufunga pekee'' , alisema mkufunzi huyo wa Man United.
''Nadhani Lukaku ni miongoni mwa wachezaji ambao hawafai kulaumiwa ama hata kukosolewa, ukiangazia swala la heshima anayofaa kupewa''.
Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji aliyeuzwa na Mourinho wakati alipokuwa mkufunzi wa Chelsea alishindwa kufunga kwa mechi ya tano mfululizo dhidi ya Tottenham siku ya Jumamosi, lakini ndiye aliyempatia pasi Anthony Martial aliyecheka na wavu.
Baada ya mechi hiyo Mourinho hakufurahia ukosefu wa kumsaidia Lukaku kutoka kwa mashabiki wa Old Trafford.
''Kwangu mimi hafai kulaumiwa katika kikosi changu na nadhani hafai kukosolewa kutokana na usaidizi anaopata kutoka kwa mashabiki'',alisema mkufunzi huyo wa Lukaku.
United inaikaribisha klabu ya Benfica nyumbani katika mechi ya vilabu bingwa Ulaya ikijua kwamba ushindi wowote utasaidia kufuzu katika raundi ya muondoano iwapo CSKA Moscow itashindwa kuilaza Fc Bazel.
No comments:
Post a Comment