Wednesday 11 October 2017

Ureno na Ufaransa zatinga Kombe la Dunia.

Ronaldo fires a left-footed shot at goal during the clash in Lisbon as Stephan Lichtsteiner attempts to make the block
Mabingwa wa Ulaya Ureno walilaza Uswizi 2-0 Jumanne mjini Lisbon na kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi kwa kumaliza kileleni Kundi B.

Iwapo wangeshindwa au kutoka sare, basi wangehitaji kucheza mechi ya muondoano kufuzu.
Lakini mabao mawili, moja la Johan Djourou aliyejifunga na Andre Silva, yalitosha kuwavusha Ureno.
Ufaransa walilaza Belarus 2-1 nakufuzu kwa kumaliza kileleni Kundi A, Swedennao wakamaliza wa pili licha ya kushindwa 2-0 na Uholanzi.
Waholanzi ambao walimaliza nafasi ya tatu Kombe la Dunia 2014 wameondolewa kwenye michuano hiyo.
Walihitaji kushinda kwa mabao saba ya wazi kuwapiku Sweden na kumaliza wa pili.
Walifunga mabao mawili pekee kuptiia Arjen Robben.
Kundi H, Ugiriki walijihakikishia nafasi michezo ya muondoano kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya Gibraltar.
Ubelgiji ambao tayari walikuwa wamejihakikishia uongozi katika kundi hilo walilaza Cyprus 4-0 huku nyota wa Chelsea Eden Hazard akifunga mabao mawili, nduguye Thorgan akafunga moja naye mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku akafunga ukurasa wa mabao.
Mataifa ya Ulaya ambayo yamefuzu kwa sasa ni Ufaransa, Ureno, Ujerumani, Serbia, Poland, England, Uhispania, Ubelgiji na Iceland.
Kuna nafasi nne zaidi za kushindaniwa na mataifa manane kupitia muondoano wa timu nane - Sweden, Uswizi, Ireland Kaskazini, Jamhuri ya Ireland, Denmark, Italia, Ugiriki na Croatia.
Uamuzi wa nani atacheza dhidi ya nani utafanywa baada ya orodha ya viwango vya soka duniani ya Fifa kutangazwa wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment