Monday, 30 October 2017

Zitto Kabwe atoa ya moyoni baada ya Lazaro Nyalandu kujivua uanachama wa CCM.

Image result for Lazaro Nyalandu,
MBUNGE wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kumpongeza aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Nyalandu ambaye leo Oktoba 30, 2017 amefanya maamuzi ya kuachana na CCM na kusema kiongozi huyo amefanya maamuzi sahihi. 


Zitto Kabwe amesema kuwa kutokana na uchumi unavyoporomoka haki za watu zinavyovunjwa jambo alilofanya Nyalandu ni sawa na kuwa huko ndiyo kuonyesha uongozi. 

“Lazaro Nyalandu, umeonyesha Uongozi. Kwa namna haki za watu zinavyovunjwa na Uchumi wa nchi unavyoporomoka, unahitaji roho ngumu Sana kuwa CCM. Umefanya maamuzi sahihi, wakati sahihi na Kwa sababu sahihi. Kila la kheri|” aliandika Zitto Kabwe 

Lazaro Nyalandu leo ametangaza kujivua nafasi zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kuandika barua yake ya kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kwa kile alichodai kuwa Chama Cha Mapinduzi na Bunge vimekuwa vikishindwa kuisimamia serikali na badala yake kutumiwa na serikali jambo ambalo yeye anaona halina afya katika maendeleo ya nchi na linadidimiza haki mbalimbali.


No comments:

Post a Comment