Wednesday 11 April 2018

Roma wamtoa Messi kichwa chini UEFA watinga nusu fainali.

Lionel Messi, wearing the captain's armband, bowed his head and looked dejected after Barcelona blew a huge advantage
Roma imefanya maajabu baada ya kuwabamiza Barcelona 3-0 na hivyo kutinga nusu fainali za mabingwa Ulaya kwa faida ya goli la ugenini.

Barca walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele kutokana na kuingia uwanjani wakiwa na akiba ya magoli, ambapo kutokana na mechi ya kwanza waliyoipiga Roma bao 4-1, Roma ilikuwa inalazimika kuifunga Barcelona 3-0.
Striker Dzeko grabbed the ball and raced back to the halfway line after his early goal sparked hope of a dramatic turnaround
Goli la Edin Dzeko dakika za awali za mchezo (6'), na Penalty ya Daniele de Rossi katika kipindi cha pili dakika ya 58 yamekamilishwa na Goli la Mlinzi Kostas Manolas alilofunga zikiwa zimesalia dakimmka nane tu mechi kufikia mwisho zimewafanya Barcelona pamoja nakuwa na Lionell Messi ambaye hakufurukuta, kuondokakichwa chini katika Ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Umati uliokuwepo Stadio Olimpico ulilipuka mara baada ya kipyenga cha mwisho pale wachezaji wa akiba wa Roma na benchi lao la ufundi walipoingia katikati ya uwanja kushangilia na wachezaji wao.
Konstantinos Manolas (centre) scored in the 82nd minute to put Roma 3-0 ahead on the night and in front on away goals
Kulikuwa na machozi katika nyuso za mashabiki wasiamini kile walichokishuhudia katika mtanange huo ambao haukutegemewa kuisha ulivyoisha.
Midfielder De Rossi kept his cool and dispatched the spot-kick beyond Barcelona's German keeper Marc-Andre ter Stegen
Roma imekuwa timu ya tatu katika Champions League kuweza kuyapindua matokeo ya namna hiyo ya goli tatu au zaidi. Timu pekee mbili ambazo awali ziliwahi kufanya hivyo ni Deportivo La Coruna dhidi ya AC Milan mwaka 2004 na Barcelona dhidi ya Paris St-Germain msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment