Wednesday 3 August 2016

Hivi ndio vyuo 5 vilivyofungiwa na NACTE kutoa huduma ya Elimu nchini huku 175 vyapewa ONYO.

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, NACTE, limevifuna vyuo 5 kutokana na kukiuka taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya usajili na ithibati

Kadhalika Baraza limetoa muda wa wiki mbili kwa vyuo 41 vinavyotoa elimu ya ufundi bila kusajiliwa kwa mujibu wa sheria vijisajili mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Akiongea na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa ,NACTE, Mhandisi Steven Mlote, amesema Baraza limetoa muda wa mwezi mmoja kwa vyuo 112 kutekeleza masharti ya usajili na vyuo 52 kutekeleza masharti ya ithibati kwa mujibu wa sheria za uendeshaji vyuo vya ufundi nchini, na vyuo vitakavyoshindwa kutekeleza agizo hili vitafungiwa mara moja.

Mhandisi Mlote ameongeza kuwa, vibali vya usajili wa vyuo 112 vya kutoa elimu ya ufundi vimefikia ukomo hivyo vinapaswa kutekeleza masharti ya Usajili; wakati vyuo 57 vimefikia ukomo wa ithibati, hivyo inapaswa kutekeleza masharti ya ithibati.

“Vyuo 175 nchini vimepewa notice ya kushushwa hadhi, 5 vimefutiwa usajili na 41 tumevifungia kuendesha mafunzo na tuna tuma timu nchi nzima kuhakikisha vyuo vya aina hii visiwepo nchini” amesema Mhandisi Mlote

Vyuo vilivyofungiwa  
State College of Health and Allied Aciences cha Dar es salaam, Zoom Polytechnic College cha Dar es salaam, Thabitha College – Dar es salaam formerly Thabita Voccational Training College cha Dar es salaam, Financial Training Centre cha Dar es salaam na TMBI College of Bisiness and Finance cha Dar es salaam.

Mhandisi Mlote ametolea mfano chuo cha State Colege of Health and Allied Sciences cha Dar es salaam kuwa huwa kama chuo mchana wakati nyakati za usiku ni klabu ya pombe hivyo mazingira yake kutofaa kwaajili ya kufundishia

"Ni lazima vyuo viwe na walimu wenye sifa ili mwanafunzi aweze kupata elimu inayostahili na cheti chake kiwe na sifa kulingana na utaratibu wa nchi hivyo mwanafunzi aliye soma kwenye vyuo hivi hata cheti chake kitafutwa ina maana kwamba akitatambuliwa wala kuruhusiwa kutumika". Amesema Mhandisi Mlote.

USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUTU FOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

2 comments:

  1. Dah masikitiko makubwa kufungwa kwa ivo vyuo kwani kumewaharibia malengo wanafunzi


    ReplyDelete
  2. Dah masikitiko makubwa kufungwa kwa ivo vyuo kwani kumewaharibia malengo wanafunzi


    ReplyDelete