Monday, 14 September 2015

TOTTENHAM ,CHELSEA WAOMBA KUTUMIA WEMBLEY

LONDON,Uingereza.

HUENDA klabu za Tottenham na Chelsea zikatumia uwanja wa Wembley kama uwanja wao wa mechi za nyumbani wakati wakifanya matengenezo ya  ujenzi wa viwanja vyao vya sasa.

Taarifa kutoka katika klabu hizo zinasema kuwa matengenezo hayo yatakayoendana na kuongeza siti kwa ajili ya mashabiki na kupanua baadhi ya maeneo katika viwanja vyao vya sasa,huenda yakawachukua muda mrefu zaidi.

Hata hivyo huenda ombi lililowakilishwa kwa chama cha soka Uingereza FA na wakurugenzi wa klabu hizo kuomba kutumia uwanja wa Wembley likakubaliwa kutokana na FA kutaka kuutumia uwanja huo kwa kama sehemu ya chanzo chao cha mapato.

Mkurugenzi mkuu wa FA,Martin Glenn amesema kuwa jambo hilo litafikishwa katika kamati husika inayihusikan na usimamizi wa uwanja huo kuona kama kunauwezekano wa kuruhusu michezo yote inayochezwa katiak uwanja huo ikapangwa tena upya ili kuhusisha baadhi ya mechi za klabu hio kutoka London.
muonekano wa ndani wa uwanja mpya wa chelsea utakavyokuwa

Klabu ya Chelsea imesema kuwa itawekeza zaidi ya pauni milioni 500 kwa ajili ya kuujenga upya uwanja wake na kuufanya kuwa na hadhi sawa na klbau nyingine kubwa.
Muonekano wa nje wa uwanja wa Tottenham

Katika mpango huo,Chelsea imeweka wazi kuwa uwanja huo utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 60,000 wakiwa wamekaa ,ampango uliopangwa kufanyika ndani ya miaka miwili kutoak hivi sasa.

Wakati Tottenham ambao wameingia makubalinao na na wamiliki wa klabu ya mchezo wa NFL kujenga uwanja mpya na wakisasa ambao pia utatumiwa kwa ajili ya michezo la ligi ya NFLwanataraji kuanza ujenzi wao katika msimu wa 2017 -18,huku wakitegemea kuwa na uwanja utakao igiza mashabiki 61,000

No comments:

Post a Comment