Tuesday, 15 September 2015

WAZIRI MKUU MPYA WA AUTRALIA HAPISHWA

AUSTRALIA

Aliyekuwa waziri wa mawasiliano katika serikali ya Abbott bw Malcolm Turnbull., sasa atakuwa waziri mkuu wa nne nchini humo tangu 2013.
“Nimejawa na matumaini tele na
tutatulia katika wiki chache zijazo. Kwa miezi michache ijayo tutaweka msingi wa mambo .yatakayotuwezesha kupata ufanisi katika miaka ijayo,” amesema.
Bw Abbott, aliyeondolewa mamlakani Jumatatu baada ya kura ya haraka kufanywa katika chama tawala cha Liberal, amesema aliondolewa kwa “uchungu” lakini ameahidi kurahisisha shughuli ya mpito kadiri anavyoweza lakini pia amekiri kuwa uchaguzi ulikuwa wa huru na wa haki.
Bw Turnbull anatarajiwa kukutana na wabunge wa chama cha Liberal na baadaye kukutana na wabunge wa muungano wa vyama vya Liberal na National vinavyotawala.
Anatarajiwa kutangaza baraza jipya la mawaziri kufikia mwisho wa wiki.

No comments:

Post a Comment