Monday, 19 October 2015

HAYA NDIO YA MOYONI KUTOKA KWA ANNA MAKINDA KUHUSU KIFO CHA DEO FILIKUNJOMBE


                                                     Spika  wa Bunge Anna Makinda
 Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh
 Anne Makinda, amemuelezea aliyekuwa Mbunge wa jimboni la Ludewa, marehemu Deo Filikunjombe, kwamba alikuwa jasiri, mchapakazi na muda mwingi aliutumia kuwajibika jimboni kwake.
Alitoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya maziko ya mbunge huyo wilayani humu jana, huku akiongeza kuwa mara nyingi baada ya vipindi vya  Bunge,       alipenda kuwahi jimboni kwake kuwatumikia wananchi.
                                              Enzi za uhai wake Deo Filikunjombe

“Filikunjombe alikuwa ni Mbunge jasiri na aliwatetea wana-Ludewa na Watanzania kwa ujumla. Alipenda kuwa karibu na wananchi…Akimaliza Bunge, alirudi haraka kwa wananchi. Kama ulikuwa naye jana jioni na asubuhi ukampigia simu, atakwambia yupo jimboni kwake,” alisema Makinda.
Alisema marehemu Filikunjombe alikuwa mbunge wa tofauti na wabunge wengine kwa utendaji kazi wake.
Aidha, Spika Makinda aliongeza kuwa marehemu Filikunjombe alikuwa ni mpiganaji na alifanya kile alichokiamini kuwa ni sahihi

No comments:

Post a Comment