Sunday, 18 October 2015

NCHI YA ZAMBIA YAFANYA MAOMBI UCHUMI USIPOROMOKE














Nchi ya Zambia yaingia katika maombi mazito  ya kuriombea taifa lao hili liweze kunusulika kuanguka kiuchumi maombi haya yameitishwa  mara baada ya kutoke kwa mfumuko wa bei kwa baadhi ya bidhaa muhimu  na baadhi ya hudumu nyingine za msimgi kitaifa
                                        Baadhi ya wananchi wa Zambia wakiwa katika maombi
Taifa hilo ambalo uchumi wake  kwa kiwango kikubwa unatokana na mauzo yatokanayo na madini ya shaba.
Thamani ya sarafu ya Zambia, Kwacha, imedorora mno na kupoteza takriban nusu ya thamani yake katika kipindi cha miezi 9 iliyopita
Kufikia sasa Sarafu hiyo imepoteza asilimia 45% ya thamani yake ikibadilishwa na dola ya Marekani.
Hali hii watafiti wa maswala ya kiuchumi wanasema imetokana na mfumuko wa bei ya shaba ambayo imeanguka mno kufuatia mfumuko katika uchumi wa mteja wake mkuu China.
                                              Raisi wa zambia Edga Lungu akiwa katika maombi

Rais Edgar Lungu anatarajiwa kuhutubia taifa hilo wakati wa hafla hiyo kubwa inayofanyika katika mji mkuu Lusaka.

No comments:

Post a Comment