WIZARA
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imebaini kuwepo kwa ongezeko la
matumizi ya ramani ya Tanzania ambayo mipaka yake imepotoshwa.
Upotoshwaji
huu umefanywa kwenye “diary” (vitabu vya kumbukumbu na matukio),
Kalenda, mabango, matangazo ya kwenye vyombo vya habari na sehemu
nyinginezo. Jambo hilo la kupotosha mipaka ni hatari kwa usalama wa
nchi.
Ili kuepusha upotoshaji wa mipaka ya nchi yetu tunashauri ramani sahihi zitumike.
Ramani
sahihi ya Tanzania inatakiwa kuonesha mpaka kwa sehemu ya maziwa ya
Victoria, Tanganyika na Nyasa ukipita katikati ya maziwa hayo.
Hivi
karibuni tumebaini matumizi ya ramani ya Tanzania kwenye majarida,
magazeti na hata Luninga inayopotosha mpaka kwa sehemu ya ziwa Nyasa
ikionesha mpaka kupita pembezoni mwa ziwa.
Kitendo
cha kuchapisha ramani yenye makosa kwa kutumia vyanzo visivyo rasmi ni
kosa kwa mujibu wa mamlaka (Instrument) ya Mhe. Waziri aliyepewa dhamana
ya kusimamia sekta ya ardhi ikiwemo masuala ya upimaji na ramani.
Idara
ya Upimaji na Ramani ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kuandaa, kuchapisha,
kutunza na kusambaza ramani zote nchini ipo tayari kutoa ramani kwa
matumizi yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu na ushauri kuhusu
usahihi wa ramani kabla ya kuitumia.
No comments:
Post a Comment