Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema anamshukuru Mungu kwa
kumuwezesha kumaliza salama utumishi wake serikalini kwenye ngazi za juu
ambao umedumu kwa takriban miaka 15.
Akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki wakati wa Ibada ya Jumapili
katika Parokia ya Mt. Anna iliyoko Hananasifu, Kinondoni jana, Pinda
alisema anamshukuru Mungu kwa kumaliza salama nafasi aliyopewa ya
kulitumikia taifa akiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na miezi tisa na
katika ngazi ya uwaziri miaka miwili na nusu na miaka mitano akiwa Naibu
Waziri.
Mh Pinda ametoa wito kwa watanzania kumtanguliza Mungu kwa kila jambo
ili kufanikisha kutatua changamoto zao, huku pia akiwasihi viongozi
waliomadarakani kutojisahau kwenda kwenye nyumba za ibada mara kwa mara
kwani wengi wao wanamsahau Mungu pale wanapokabidhiwa madaraka.
Mizengo Pinda akiwa Bungeni
Monday, 19 October 2015
PINDA:NAFURAHI KUMALIZA SALAMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment