Tuesday 3 November 2015

Listi yote ya waliochukua Tuzo mwanasoka Bora Barani Afrika

Image result for mchezaji wa ivory coast yaya toure
Kiungo wa kati wa Ivory Coast  na club ya matajiri wa london manchester city Yaya Toure yumo miongoni mwa wachezaji 10 walioteuliwa kushindania tuzo ya Mchezaji wa Mwaka wa Shirikisho la Soka barani Afrika, hii ikiwa mara ya tano mtawalia.
Orodha hiyo ilitolewa na Caf Jumatatu.
Mchezaji huyo wa miaka 32 anayechezea Manchester City ya Uingereza alishinda tuzo hiyo mara ya kwanza 2011 na akishinda mwaka huu itakuwa mara yake ya tano.
Image result for samuel eto'o
Akifanikiwa kutwaa tuzo hiyo, atakuwa amempita Samuel Eto'o ambaye ameshinda tuzo hiyo mara nne.
Mshindi ataamuliwa kwa wingi wa kura zitakazopigwa na makocha au wakurugenzi wa kiufundi wa mataifa wanachama wa Caf.
Tuzo hiyo itatolewa kwenye hafla itakayoandaliwa Alhamisi, Januari 7, 2016 mjini Abuja, Nigeria.
Orodha kamili 
  1. Andre Ayew (Ghana & Swansea)
  2. Aymen Abdennour (Tunisia & Valencia)
  3. Mudather Eltaib Ibrahim 'Karika' (Sudan & El Hilal)
  4. Mohamed Salah (Egypt & Roma)
  5. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund)
  6. Sadio Mane (Senegal & Southampton)
  7. Serge Aurier (Cote d'Ivoire & Paris Saint Germain)
  8. Sofiane Feghouli (Algeria & Valencia)
  9. Yacine Brahimi ( Algeria & Porto)
  10. Yaya Toure (Cote d'Ivoire & Manchester City)

No comments:

Post a Comment