Sunday, 8 November 2015

Mwanaume mmoja nchini marekani Atorewa minyoo kichwani



Mwanamume mmoja nchini Marekani anazidi kupata afueni baada ya kufanyiwa upasuaji wa kumuondoa minyoo kutoka ndani ya ubongo wake.
Luis Ortiz alilazwa katika hospitali eneo la Napa mjini Carlifonia baada ya kuugua maumivu ya kichwa aliyotaja kuwa baya zaidi maishani mwake.
Daktari Soren Singel aliyefanya upausaji huo, alimkagua na kupata yai la minyoo na kumuambia Ortiz alikuwa na dakika 30 tu za kishi.
Minyoo hiyo ilikua katika uvimbe uliyokatiza usambazaji wa maji maji muhimu kwenye ubongo wake.
‘’Nilishtuka kisha nikatapika. Alisema Ortiz.
"Daktari aliitoa na kusema ilikuwa hai.





minyoo iliyotolewa kichwani
 

Kituo cha Marekani cha uzuiaji na udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza yaani CDC kimeripoti kuwa uvimbe wa mabuu kwenye ubongo yaani 'neurocysticercosis' hutokea baada ya mtu kumeza mayari madogo yanayosambazwa kupitia kinyesi cha mtu mwenye minyoo mara nyingi kutokana na ulaji wa nyama ya nguruweya tumbo inayotokana na nyama ya nguruwe.
Mayai hayo yakiwa mwilini huangua minyoo inayoweza kuingia kwenye ubongo.
Kulingana na CDC, zaidi ya watu 1000 hulazwa hospitalini kutokana na 'neurocysticercosis' na uondoaji wa mabuu yake (larvae).
Ortiz anazidi kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji mwezi Novemba na anatarajia kurudi katika chuo kikuu cha Sacramento anakotarajiwa kuendelea na masomo yake ya mwaka wa nne.
‘’Kuwa hai ni faraja kwangu kwa sababu kama ningesubiri zaidi pengine singekuwa hapa kwa sasa'' aliiambia shirika la CBC San Francisco.

No comments:

Post a Comment