Wednesday 4 November 2015

Raisi kikwete azungumza na mgombea wa urais Zanzibar Sharif Hamad















Mh.DKJakaya kikwete  akizungumza na mgombea wa uraisi zanzibar Mh. Sharif Seif Hamad

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo Jumatano, Novemba 4, 2015, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha Civic United Front (CUF), Mheshimiwa Seif Shariff Hamad ambaye pia alikuwa Mgombea Urais wa Zanzibar wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uliofanyika Oktoba 25.
 Viongozi hao wawili walikutana kwa kiasi cha saa moja Ikulu, Dar es salaam, kuzungumzia hali ya kisiasa Zanzibar kufuatia ombi la Mheshimiwa Hamad kutaka kukutana na kuzungumza na Rais Kikwete.Viongozi hao wamekubaliana kuwa mashauriano yaendelee kufanyika baina ya pande zote zinazohusika na hali ya kisiasa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment