Saturday 7 November 2015

Tanzania yaitaka china kuhimalisha mahusiano ili kukuza uchumi na biashara

 












Rais Dkt.John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala Cha China Mhe.Zhang Ping Ikulu jijini Dar es Salaam

Tanzania imeitaka China kuimarisha uhusiano baina ya nchi zao kwa kuisaidia Tanzania kukua zaidi kiuchumi na kibiashara ili kuweza kutimiza azma ya viongozi wa Tanzania ya kuwaletea watanzania maendeleo zaidi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amesema hayo leo, Ikulu alipokutana na Ndugu  Zhang Ping, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Kikomunist cha China (CPC), ambacho ndicho chama tawala nchini humo.
“Tuimarishe uhusiano wetu kwa misingi ya kuufanya uwe uhusiano wa kuisaidia Tanzania kunufaika kiuchumi na kibiashara ili kuweza kutimiza azma yangu ya kuwaletea watanzania maendeleo”. Amesema Rais Magufuli ambaye amekutana na Ndg. Ping aliyekuja nchini kumuwakilisha Rais wa China katika sherehe za kuapishwa Rais Magufuli tarehe 5 Oktoba, 2015.
Rais Magufuli amekutana na viongozi wengine ambao pia waliwakilisha viongozi wa nchi zao katika sherehe hizo.
Wawakilishi hao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Algeria Ndg. Ramtane Lamamra, Ndg. Pascal Nyabenda, Spika wa Bunge la Burundi na Waziri wa Kilimo wa Misri Ndg. Essam Fayed.
Mapema asubuhi Rais Magufuli amemuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndg. George  Mcheche Masaju na kisha kuendelea na kazi zake za kiofisi.

Rais Magufuli amewataka watumishi wote kufanya kazi zao kwa uadilifu, kwa bidii na kujituma zaidi ili kuweza kuwatumikia watanzania na kuweza kutimiza mategemeo yao ya kuletewa maendeleo na kukua kiuchumi

No comments:

Post a Comment