Thursday, 28 April 2016

Kauli ya Waziri mkuu kuhusu mikataba ya Serikali na Bunge hii hapa

IMGS0934
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim amesema kwamba siyo mikataba yote serikali inaingia na taasisi mbalimbali hupelekwa bungeni.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo bungeni baada ya Mbunge wa Viti maalum Chadema Kunti Majala kuuliza swali kwamba kuna mikataba ambayo inatekelezwa nchini na serikali wakati bunge halikupitisha mikataba hiyo.

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu Majaliwa amesema kwamba kama bunge lingekuwa linapelekewa mikataba yote basi lingefanya kazi ya kushughulika na mikataba tuu.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaruhusiwa kusaini mikataba ya nchi kwa niaba ya serikali hivyo hakuna kosa lolote serikali imefanya kwa kutopeleka mikataba hiyo bungeni.

Bunge la 11 mkutano wa tatu kikao cha saba limeendelea leo ambapo serikali imeweza kutoa majibu ya maswali kwa wabunge kutoka maeneo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment