Akiongea wakati wa uwasilishwaji wa ripoti hiyo kwa waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, mshauri mwandamizi wa mawasiliano wa tasisi ya TWAWEZA Risha Chande amesema, Takribani wananchi kati ya wanane na kumi ambao ni sawa na asilimia 78 wanaamini upatikanaji wa habari unapunguza vitendo vya rushwa, huku wanachi kati ya sita na kumi ambao ni sawa na asilimia 68 wamependekeza serikali iwe na mamlaka muhimu ya kuzuia habari zinazotishia usalama wa Taifa.
Aidha, ripoti hiyo pia iligusia hali ya upatikanaji wa habari kutoka taasisi za umma kwa wananchi ambapo zaidi ya wananchi kati ya wanane na kumi walio hojiwa katika ripoti hiyo wamesema hawajawahi kufika katika ofisi za mamlaka ya Maji, shule za Umma, vituo vya Afya wala ofisi za serikali za mitaa kutafuta taarifa zozote nakuwa wananchi wengi wakitegemea vyombo vya habari mbalimbali kupata taarifa kutoka taasisi hizo.
Richa amesmea Redio inaaminika na asilimia 80 ya wananchi, runinga (TV) inaaminika na asilimia 73 ya wananchi, tofauti na magazeti ambayo yanaaminika kwa asilimia 27 tu ya wananchi. Japokuwa mitandao ya kijamii inaaminika kwa kiasi kidogo sana na kutumiwa kwa kiwango cha chini kama chanzo cha habari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, anasema “Kwa kiasi kikubwa wananchi wanaunga mkono uwepo wa uwazi wa taarifa. Vilevile wameweka wazi vyanzo vya habari wanavyovitumia na kuviamini. Ni vema kufahamu kwamba wananchi wenye taarifa, na uhakika kwamba mawazo yao yatapokelewa, kufanyiwa kazi, na kuleta mabadiliko, wanao uwezo mkubwa wa kushiriki vizuri katika kutekeleza mipango kabambe ya serikali ya awamu ya tano
No comments:
Post a Comment