Thursday, 28 April 2016

Zifahamu Saa ghali zaidi Duniani kwa mwaka huu 2016 hapa(+picha)

 
Je unamiliki saa ?
Ilikugharimu shilingi ngapi kuinunua saa hiyo?

Punde baada ya maafisa wa kupambana na ufisadi nchini Nigeria kutangaza kuwa wamenasa mapambo yenye thamani ya dola milioni 2 nyumbani kwa aliyekuwa waziri wa mafuta wa nchi hiyo bi Diezani Alison Madueke watu wengi wameelezea mshangao wao kutokana na thamani hiyo ya juu ya saa hiyo.
Wengi kupitia kwa mitandao ya kijamii wanahoji itakuwaje saa inagharimu fedha za aina hiyo ?
Kwani saa hiyo imeundwa na nini ?
Haya basi
Utafiti unaonesha kuwa .
1.) Saa yenye thamani ya juu sharti iwe na sehemu zilizoundwa na mawe yenye thamani ya juu kama vile Almasi, Platinum, dhahabu, na mawe kutoka anga ya mbali.
2.) Saa hiyo lazima iwe imechukua muda mrefu sana kuitengeneza na iwe na uwezo wa kufanya kazi bila hitilafu ya mara kwa mara
3.) Saa hiyo pia lazima iwe na uwezo wa kipekee wa kutekeleza majukumu yake mbali na kueleza wakati
Hivyo ndivyo vipengee tatu muhimu ambavyo vinajirejelea katika orodha ya saa tano ghali zaidi duniani mwaka huu wa 2016 kulingana na jarida la saa ghali zaidi la ALUX.
Hii hapa ni orodha ya saa 5 yenye thamani ya juu zaidi duniani.
5. LOUIS MOINET METEORIS Bei: $4.600.000
Saa hii ni ya kipekee sana.
Ukiitaka sharti uwe na uwezo wa kulipa nauli ya roketi kwenda hadi kwenye mwezi ilikuchukua mawe ambayo itachongwa ilikuunda sehemu muhimu ya saa hii.
Hii ni baadi ya saa nne duniani ambazo zinasehemu muhimu zinazotoka katika anga ya mbali.
Saa hii ni nadra sana hivi kwamba watengenezaji wake yaani Louis Moinet hufunga safari hadi anga ya mbali kuchukua vipuri vya saa hizi zenye nembo ya Meteoris
Kati ya saa hizo nne 3 ndizo zenye thamani ya juu zaidi duniani.
4. HUBLOT – BIG BANG Bei: $5.000.000
Kinyume na ile saa iliyoshikilia nafasi ya 5 yenye vipuri kutoka anga ya mbali, saa hii imeshikilia nafasi ya 4 kutokana na almasi.
Ukweli ni kwamba saa hii ya kipekee imeundwa kwa alamasi.
Saa hii aina ya Hublot -Big bang imeundwa kwa kuunganisha Almasi 1280 zenye ubora wa karati 3 kila moja.
Ilichukua mwaka mmoja wa kukata na kutayarisha Almasi hiyo inayotisha kutengeneza saa moja ya Big Bang.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Beyonce Knowles aliinunua saa hiyo na kumzawadi mumewe Jay Z katika sherehe ya kuadhimisha miaka 43
 
Kwa sasa najua unataka kujua iwapo saa yenye thamani hiyo ya dola milioni $5 inapata mteja.
Bila shaka.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Beyonce Knowles aliinunua saa hiyo na kumzawadi mumewe Jay Z katika sherehe ya kuadhimisha miaka 43.
3. PATEK PHILIPPE – HENRY GRAVES Bei: $11.000.000
Saa hii ya Henry Graves ilikuwa saa iliyoweka rekodi ya kuwa ghali zaidi duniani kwa kipindi kirefu.
Hata hivyo saa hii iliuzwa kwa bei ya dola milioni $9 mwaka wa 1999.
Amini usiamini saa hii ilitengenezwa mwaka wa 1933 mahsusi kwa ajili ya bwenyenye mmiliki wa benki bwana Henry Graves.
Mtengenezaji wake bw Patek Philippe anasema ilimchukua miaka 5 kuikamilisha saa hiyo ya kipekee.
Imejijengea sifa ya kuwa saa ya pekee duniani yenye uwezo wa kutekeleza majukumu 24 kwa wakati mmoja.
Henry Graves iliundwa kutokana na dhahabu.
Dhahabu yenye ubora wa karati 18.
Hadi mwaka wa 2013 hakuna saa yeyote iliyowahi kuishinda saa hiyo kwa ubora.
2. CHOPARD 201- CARAT Bei: $25.000.000
Saa inayoshikilia nafasi ya pili duniani katika orodha ya saa 5 bora duniani ni saa ya Chopard 201- Carat.
Saa hii yenye thamani kubwa zaidi duniani katika kitengo cha mapambo imeundwa kutokana na almasi 874 nadra zaidi duniani.
Iliuzwa mwaka wa 2000 kwa thamani ya dola milioni $25.
Wakati huo bei yake iligonga vichwa vya habari kote duniani.
Tofauti na saa ya kawaida , CHOPARD 201- CARAT haina umbo maalum kwani almasi imeunganishwa tu kiholela bila kuzingatia hali halisia ya matumizi yake.
Chopard ina Almasi za kipekee kadhaa
Soma orodha kamili ya Almasi:
– 1 almasi yenye umbo la moyo na rangi ya waridi , karati 15.37. – 1 Almasi yenye umbo la moyo,na rangi ya samawati, karati 12.79. – 1Almasi yenye umbo la moyo yenye rangi ya D,Karati 11.36. – 3 Almasi zenye umbo la tunda rangi ya njano karati, 8.45 . – 26 Almasi zenye umbo la tunda rangi ya Njano Karati, 17.07 – 48 Almasi zenye umbo la mduara rangi ya njano karati, 8.81 – 260 Almasi zenye umbo la tunda rangi ya D karati 60.94 – 91 Alamsi zenye umbo la mduara rangi ya, D karati 10.29. – 443 FC Almasi za FC za rangi ya manjano karati, 4.95
1. BREGUET GRANDE COMPLICATION MARIE-ANTOINETTE Bei: $30.000.000Saa yenye gharama ya juu zaidi mwaka wa 2016 ni BREGUET GRANDE COMPLICATION ya MARIE-ANTOINETTE.
Amini usiamini saa hii inagharimu dola milioni $30m.
Saa hii ya kipekee ilichukua miaka 34 kuundwa.
Yamkini aliyeagiza saa hii itengenezwe alikuwa ni mpenzi wa malkia wa Ufaransa wakati huo bi Marie Antoinette.
Yeye mwenyewe hakuwahi kuiona ama hata kuitumia saa hii kwani ilikamilishwa muda mrefu, miaka 34 baada yake kupigwa risasi na kuuawa.
Abraham-Louis Breguet alipokea agizo la kutengeneza saa hiyo mwaka wa 1782 hata hivyo aliaga dunia na ikambidi mwanaye akamilishe kazi hiyo 1827 miaka minne baada ya kifo chake.
Saa hii ya dhahabu iliwavutia wengi sana wakati huo.
Aidha ilikuwa imekamilika wakati huo na hata sasa bado inamshiko.
Moja ya sababu inayoipa thamani kubwa ni kuwa bado inaweza kutekeleza majukumu yake kikamilifu zaidi ya karne 2 baada ya kuundwa.
Saa hiyo iliibiwa mwaka wa 1900.
Hata hivyo ilipatikana mwaka wa 2007.
 
         Abraham-Louis Breguet alipokea agizo la kutengeneza saa hiyo mwaka wa 1782
Saa hiyo kwa hivi sasa inalindwa na makavazi ya kitaifa ya L. A. Mayer nchini Israeli.
Saa hii ndiyo ghali zaidi mwaka huu 2016

No comments:

Post a Comment