Tuesday 26 April 2016

Rais Magufuli atoa pole kwa Familia ya Kibaki

Mama Lucy Kibaki ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki amefariki dunia Jijini London nchini Uingereza, ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Katika salamu hizo Rais Magufuli ameelezea kushtushwa na kifo hicho na kuongeza kuwa Kenya imempoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yake.
“Kupitia kwako Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta napenda kumpa pole nyingi Rais Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki, Familia yake, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote walioguswa na msiba huu mkubwa” Amesema Rais Magufuli.
Dkt. John Pombe Magufuli pia amemuombea marehemu Lucy Kibaki apumzishwe mahali pema peponi, Amina.

No comments:

Post a Comment