Rais wa Tanzania John Magufuli
amependekeza daraja mpya la Kigamboni lipewe jina la mwanzilishi wa
taifa hilo Mwalimu Julius Nyerere.
Akiongea muda mfupi kabla ya
kuzindua rasmi daraja linafaa kupewa jina la Mwalimu Julius Nyerere
kutokana na mchango wake kwa nchi hiyo.
Daraja la Kigamboni
lilianza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 na lina urefu wa mita 680 na
barabara unganishi upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa
kilomita 2.5.
Ujenzi wake ulifanywa na kampuni ya China Railway 15 Group ikishirikiana na kampuni ya China Bridge Engineering Group.
Daraja
hilo ndilo la kwanza la kubeba uzito wa barabara kwa kutumia nyaya
Afrika Mashariki na la tatu Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara bila
kuhesabu Afrika Kusini.
Linamilikiwa na serikali ya Tanzania na
Hazina ya Malipo ya Uzeeni (NSSF) kwa 40% na 60% mtawalia na litachukua
nafasi ya feri ya MV Magogoni.
Ujenzi wa daraja hilo, ambao uligharimu dola 128 milioni za Kimarekani, ulianza mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment