Tuesday 19 April 2016

Ripoti mpya ya Tume ya Uchaguzi ya Tanzania kuhusu uchaguzi 2015

 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC leo imetoa hati za shukrani kwa wadau walioshiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa kutambua mchango wao.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hati hizo mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema Tume inatambua mchango mkubwa uliotolewa na wadau wa uchaguzi kwani Tume peke yake isingeweza kufanya kazi hiyo.

Jaji Lubuva amesema uchaguzi umemalizika hivyo ni vema sasa wananchi kushikamana kwa pamoja kitaifa ili kuendelea kuijenga nchi kwa amani na upendo.

Waliokabidhiwa hati hizo ni vyama vyote vya siasa pamoja na wadau wengine ambao walishiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment