Monday 25 April 2016

Wazazi walalamikia Ugonjwa wa Selimundu (SICKLE CELL) kusitishwa kwa huduma za tiba bure


 


Wazazi wenye watoto wenye ugonjwa wa selimundu (SICKLE CELL) wamelalamikia kusitishwa kwa huduma za tiba za bure kwa watoto hao katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.

kitendo ambacho wamesema kitadumaza afya za wenye tatizo hilo ambao wengi  wao hawana fedha kumudu matibabu hivyo kuiomba serikali kuangalia namna ya kuendeleza huduma hiyo.

Wakizungumza na waandishi wa habari wazazi wa watoto hao wamesema walikuwa wakipatiwa huduma za tiba, vipimo na ushauri bure katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam lakini ghafla mwezi huu wameambiwa kuwa huduma za bure za ugonjwa wa SICKLE CELL katika hospitali hiyo hazitatolewa tena na baadhi yao kupangiwa kuhudhuria kliniki katika hospitali za Amana na Temeke huku wakilalamikia hospitali hizo kukosa kitengo maalum cha matatizo ya seli mundu.

Wamesema mpaka sasa kati ya wagonjwa elfu sita wa sickle cell waliokuwa wakipatiwa huduma katika hospitali hiyo mia saba tayari wamepangiwa rufaa kwenda kupata huduma katika hospitali za Temeke na Amana zote za jijini Dar es salaam.

Kwa upande wa Hospitali ya taifa ya Muhimbili wameelezea kuwa huduma hiyo ilikuwa chini ya mradi wa utafiti uliokuwa ukifanywa kati ya Chuo cha afya cha Muhimbili na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, mradi ambao umefikia mwisho tarehe 31 mwezi wa tatu hivyo matibabu ya SICKLE CELL yataendelea kwa utaratibu wa kawaida na sio chini ya mradi huo wa utafiti.

Ugonjwa wa siko seli, mtoto hurithi vinasaba vya seli mundu (sickler DNA) kutoka kwa wazazi wote, ni ugonjwa wa kurithi unaoathiri seli nyekundu za damu mwilini ambapo huathiri sana watu wenye asili ya Afrika, pia wale wenye asili ya Mashariki ya Kati, kihispania na Asia, ambapo Tanzania inashika nafasi ya nne kwa nchi zinazoongoza kuwa na tatizo hilo zikiongozwa na Nigeria, Congo, Angola na Tanzania ikishika nafasi ya nne.

No comments:

Post a Comment