Monday 25 April 2016

Zaidi ya kaya 400 katika wilaya ya Moshi kusombwa na Mafuriko

 
Zaidi ya kaya 400 katika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro ,hazina mahala pa kuishi kufuatia mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha yaliyozijumba nyumba zao huku paa za baadhi ya nyumba zikiezuliwa.


Mvua hizo pia zimeharibu mazao mashambani hususan  mahindi, migomba maharage na mpunga ,sambamba na miundombinu ya barabara na madaraja hivyo kusababisha wananchi wakose mawasiliano kutoka eneo moja  kwenda jingine.

Wakizungumza wakati mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadik alipotembelea maeneo yaliyoathirika na mvua hizo, baadhi ya wananchi na viongozi wa maeneo hayo wamesema licha mafuriko hayo kuharibu miundo mbinu na mashamba yenye mazao, pia yamesomba vyakula,nguo pamoja na mifugo ikiwemo  kuku na bata.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadik akizungumza baada ya kutembelea maeneo  hayo amesema serikali itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha misaada ya haraka ya kibinadamu inapatikana huku akiwataka wakurugenzi na wakuu wa wilaya kuhakikisha wanazuia ujenzi holela wa nyumba katika maeneo ya mapito ya maji.

Baadhi ya maeneo yaliyoathirika na mafuriko hayo ni ,kata ya Msaranga, mandaka mnono ,njoro ,na kilema kusini maeneo mengine ni kata ya kahe ,miwaleni pamoja na  kisangesangeni,ambapo baadhi ya nyumba zimebomoka,huku vyakula na mifugo kusommbwana maji  ,pia uharibifu wa miundombinu ya barabara na madaraja.

No comments:

Post a Comment