
Balozi wa China hapa nchini Lu Younging amesema kasi ya ukuaji uchumi wa taifa imeongezeka kutokana na ukuaji wa teknolojia ambao umechangia katika kurahisisha upatikanaji wa huduma hususani za kifedha kwa wafanyabiashara baina ya nchi na nchi.
Balozi Younging alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo wa malipo wa China unaojulikana kama Umoja Pay ambao utawezesha wafanyabiashara kutoka China wakiwa nchini kupata huduma za kifedha kupitia umoja switch kutumia kadi zinazotumia mfumo huo, ambapo wataweza kutoa fedha kwenye ATM za umoja switch huduma ambayo inapatikana dunia nzima.
Amesema hatua hiyo sasa inaiweka Tanzania miongoni mwa nchi ambazo zitawavutia zaidi wafanyabiashara.
Akizungumzia mfumo huo afisa mtendaji mkuu Umoja Switch Danford Mbilinyi amesema utaongeza idadi ya wafanyabiashara na kwamba mipango ya baadaye ni kuwawezesha watanzania kutumia kadi za umoja switch katika ATM zote duniani ziliounganishwa kwenye mradi huo.
No comments:
Post a Comment