Sunday 8 May 2016

Hatupangi kushindwa tushindwa kupanga,Fahamu hatua za msingi za maendeleo katika Maisha

 
Kupanga ni kujiandaa kujiandaa ni siri ya mafanikio “kama ningekuwa na  masaa sita ya kukata miti ningetumia masaa manne ya kwanza kunoa shoka” alisema  Abrahamu Lincolin.

Kutojiandaa ni kutokuwa tayari kuna kujiandaa kisaikolojia ,kiroho na hata kimwili pia kwa mfano ukienda kula unanawa mikono  ni kujiandaa kimwili, mwanafunzi anapaswa kujiandaa kwa ajili ya mtihani na anae  taka kuoa lazima ajiandae 
 
Usikate kanzu kabla ya mtoto hajazaliwa
Ni msemo ambao unatuweka katika utamaduni wa kutopanga kabisa ya kesho. Katika maisha ya kawaida hapa afrika mambo mengi yanatujia bila kuyapangilia ,mzazi atahangaika sana kutafuta karo ya mtoto kama anajiunga na chuo kikuu miaka yote wakati mtoto anakua na kupanda darasa kila mwaka mzazi au mlezi wa mtoto huyo hakupanga ya mbele

Utamaduni wa kupanga

Mzazi anaposhindwa kupata karo, je alipanga kushindwa kupata karo au alishindwa kupanga, hata baadhi ya wakulima hutegemea mvua inyeshe hata kama hawajaandaa shamba mahali pa kupanda mbegu kama za mahindi au maharagwe, hii  ni kasoro na ukosefu wa utamaduni. Wakupanga  mambo ya kesho  ambao unasisitizwa hata katika vitabu vya dini, kutathimini ulionayo au kukadiria ghalama za maisha ni siri katika kupanga ya kesho biblia ina tushauri kuwa na utamaduni wa kukaa na kupanga mambo ni vizuri yawe hivyo katika maisha ya kila siku kuna aina mitindo au vielelezo mbalimbali  vya kupanga mambo ya kesho kijamii,kidini,kiuchumi na hata kisiasa ,kuna mitindo mingi ya kupanga mambo kwa siku zijazo.  

Kupanga kutokana na mazuri ulionayo

Kupanga kutokana na rasilimali ulizonazo uwezo ulionao ,mali ulizonazo,maliasili ulizonazo nyenzo ulizonazo au kimbilio ulionalo,tegemeo ulilonalo au watu ulionao mfano kuwa nawa Tanzania wanaoishi nchi za nje  ni nguvu ya kuanzia kupanga  ya kesho.Basi kuwapo na mikakati na mipango ya kuwafanya wanaoishi nchi za nje wawekeze zaidi nchini mwao,kwani waswahili usema upendo huanza nyumbani ingawa lazima utoke na kuhudumia wengine.

Kupanga kutokana na nyufa ulizonazo

 “usipoziba ufa utajenga ukuta” huu ni msemo unaomaanisha kuwa usipo rekebisha tatizo dogo basi jiandae kutatua matatizo makubwa zaidi yaliotokana na tatizo dogo,kasoro unazoziona katika shughuli zako  au udhaifu ambao ni kikwazo kwa mafanikio ni vizuri kuzikabili ili zisije kukukwamisha hapo baadae.

Kusoma alama za nyakati

Ni muhimu kusoma alama za nyakati za sasa na kupanga ya keshoni kuwa na ndoto inayoendana na hali halisi ya mambo.

No comments:

Post a Comment