Monday, 9 May 2016

Haya ndio maamuzi ya Serikali kuhusu akaunti zake benki za biashara

 
Mashirika na Taasisi zote za Serikali zimetii agizo la serikali la kufunga akaunti zake katika benki za kibiashara na kuhamisha fedha zilizopo kwenye akaunti hizo kwenda akaunti walizoamriwa kufungua kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
    Msajiri wa Hazina Bw. Lawrence Mafuru.
Hayo yamebainishwa mwishoni mwa wiki na Msajili wa Hazina Bw. Lawrence Mafuru, baada ya kutoa agizo hilo la kuwapa muda kukamilisha kufungua akaunti hizo, mashirika na taasisi zote zaidi ya 200 walianza mchakato ndani ya muda husika.

Bw. Mafuru amesema kuwa mpaka sasa kuna Taasisi au Mashirika chini ya 50, ambayo hayajakamilisha uhamishaji wa akaunti zao kwa akaunti hizo kwa sababu mbalimbali ikiwemo zilizo katika mikoa ambayo hakuna tawi la BOT.

Bw. Mafuru amesema akaunti nyingine za mashirika na taasisi hizo, ziko katika akaunti za muda maalum katika benki hizo za biashara, hivyo kabla ya kuvifunga na kuhamisha fedha husika, kutahitajika majadiliano kati ya shirika au taasisi husika na benki yake.

No comments:

Post a Comment