Saturday 7 May 2016

Hivi ndivyo Walimu Wanavyofanya Kazi mkoani Geita

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida walimu wa shule ya msingi nguzo mbili ilioko kata ya Buhalahala wilaya na Mkoa wa Geita
wanalazimika kufanyia kazi zao chini ya miti kwa kile kinachodaiwa kukosa Ofisi kwa muda mrefu huku vyumba vya madarasa na madawati ikiwa ni changamoto kubwa.

walimu
Wametoa kauli hiyo baada ya kutembelewa na kituo cha  Channel Ten iliyofika katika shule hiyo majira ya saa mbili asubuhi na kukuta walimu wakiwa wanaendesha kazi zao chini ya miti, ambapo wametoa kilio chao.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Grace Kibumo amesema changamoto hizo za kukosa Ofisi na vyumba vya madarasa ni muda murefu sasa na kuiomba serikali kuimaliza.

Shule hiyo yenye wanafunzi 2771 huku vyumba vya madarasa vikiwa saba na huku walimu na wanafunzi wakitumia matundu manne kwa kuchangia

No comments:

Post a Comment