Saturday, 7 May 2016

Upungufu wa Damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wasababisha CHADEMA kufanya maamuzi haya.



Hospitali ya Taifa ya Muhimbili bado inakabiliwa na upungufu mkubwa wa damu kuweza kusaidia wahitaji wanaofika katika Hospitali hiyo ya rufaa,ambapo imesema,wakati mahitaji halisi kwa siku
yakiwa ni yuniti 80 mpka 100,ni yuniti 20 mpaka 40 pekee zinapatikana kutokana na njia ikiwamo ya ndugu wa muhusika,kutakiwa kumtolea damu mgonjwa wao.

Upungufu huo umebainishwa na Afisa Uhusiano wa Hospitali hiyo,NEEMA MWANGOMO,wakati wa zoezi la kujitolea damu katika hospitali hiyo lililoendeshwa na Chama Cha Demorasia na Maendeleo,Dar Es Salaam kuu, ikiwa ni kuuunga mkono makundi mbali mbali ya wahitaji wakiwemo akina mama,watoto na wanaogua saratani.

damuAfisa Uhusiano huyo aidha ametoa wito kwa wananchi mmoja mmoja,makundi ama taasisi,kujitokeza kujitokeza kujitolea damu kuweza kusaidia makundi hayo, hususani kipindi inapoendesha zoezi la upasuaji moyo watoto kwa ushirikiano na wataalamu kutoka Saudi Arabia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chadema Dar Es Salaam kuu,HENRY KILEO,ametoa wito kwa vyama vingine vya siasa kuwa na utaratibu wa kuhamasishana kujitolea damu kuokoa maisha ya wananchi,kama vile wanavyohamasishana wakati wa kampeni

No comments:

Post a Comment