Wednesday 4 May 2016

Huu ndio mkakati wa Serikali kuhusu kurekebisha shule zote kongwe nchini.

Serikali imesema kuwa iko katika mkakati wa kuhakikisha shule zote kongwe nchini zinarudi katika hali yake ya kawaida ambapo itaanza na baadhi ya shule nchini ili kuboresha Sekta ya Elimu nchini.
Akizungumza Mjini Dodoma, mara baada ya kufanya ziara katika shule kongwe ya Sekondari ya Mpwapwa, Naibu Waziri wa TAMISEMI,Mhe. Suleiman Jaffo, amesema ameshangazwa na shule hiyo kuwa na tatizo la maji lililodumu kwa muda mrefu kwa kukosa shilingi milioni nne.

Baada ya kushuhudia tatizo hilo Naibu Waziri huyo ametoa muda wa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, kuhakikisha anatatua tatizo hilo la maji katika shule hiyo.
Mhe. Jaffo amesema kuwa ni jambo la aibu kwa taasisi kama hiyo kukosa fedha ya kutatua tatizo hilo kwa muda wa mwaka mmoja huku akitoa agizo la kufanya marekebisho ya bweni ambalo liliteketetea kwa moto na halijafanyiwa marekebisho yoyote.

Amemuagiza Mkurugenzi huyo kupita kwa wadau wa elimu kuweza kuchangia ujenzi wa baadhi ya miundombinu ya shule hiyo lakini pia wasimamie shughuli hizo ipasavyo kwa kuwa watumishi wengi wasiposimamiwa hawafanyi kazi zao

No comments:

Post a Comment