Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limewaua kwa risasi watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi na kukutwa na bunduki moja aina
ya AK 47 ikiwa na risasi kumi na nane milipuko ishirini na saba sale za jeshi la wananchi wa Tanzania na bendera inayodaiwa kutumiwa na kikundi cha Al Shababu katika tukio lililotokea eneo la Engosheraton Sinoni jijini Arusha.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha Libaratus Sabas amesema
jeshi la polisi lilipata taarifa ya uwepo wa majambazi hao kutoka kwa
wasamariawema wakitaka kufanya tukio na baada ya kufika katika eneo la
tukio watu hao walianza kurusha risasi kwa askari lakini askari
waliwashinda nguvu na kufanikiwa kuuwa majambazi watatu ambapo mmoja
akifaamika kwa jina la Athumani Ramadhani.
No comments:
Post a Comment