Tuesday 3 May 2016

Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kuendelea kesho Azam FC na JKT kusaka pointi tatu

Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inaendelea tena hapo kesho kwa kupigwa kwa mchezo mmoja utakaowakutanisha Azam FC wakiwakaribisha JKT Ruvu Uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam.

Afisa habari wa Azam FC, Jaffery Iddy Maganga, amesema mchezo uliopita dhidi ya Simba kikosi hakikuwa kizuri kwani wachezaji walikuwa na uchovu lakini wanaamini katika mchezo wa hapo kesho wataingia kwa nia moja ya kupambana ili kupata pointi tatu.
 
Jaffery amesema, anaamini mchezo huo utakuwa mgumu kwani JKT inapambana ili isiweze kushuka daraja kwani kwa sasa ipo katika nafasi mbaya huku wao wakiwania kupata pointi tatu za kuwaweka katika nafasi nzuri zaidi katika msimamo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.

Maganga amesema, wachezaji waliokuwa majeruhi watarudi hapo kesho kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi isipokuwa Mlinzi wao FC Pascal Wawa ambaye bado ni majeruhi lakini akiwa ameanza mazoezi madogo madogo.

No comments:

Post a Comment