Vijana wadogo wenye umri kati ya miaka 14- hadi 16 wanaojihusisha na Vikundi vya Uporaji maarufu panya road wapatao 76 wametiwa mbaroni na jeshi la Polisi katika maeneo ya mbande mbagala jijini dsm wakati wakifanya matukio ya Uporaji huku wakiwa na mbwa zaidi ya wanane ambao wamekuwa wakitumika katika matukio ya Uporaji na Unyang’anji.
Kamanda wa Polisi kanda maalum CP Simon Siro amesema vijana hao wamekuwa wakifanya matukio hayo kuanzia majira ya saa 12 jioni katika maeneo mbali mbali huku wakitumia mapanga na visu ili kufanikisha Uporaji.
Aidha Kamanda Siro amesema jeshi hilo pia limewatia mbaroni watuhumiwa watano wa ujambazi pamoja na silaha tatu, mbili bastora mbili na bunduki aina ya short gan moja ambazo zimekuwa zikitumika katika matukio ya unyang’anyi ambapo pia wamefanikiwa kumkamata Edward Milingo mkazi wa majumba sita kwa wizi wa hivi karibuni wa magari matatu.
Katika kupambana na Usafirishaji haramu wa binadamu Kamanda siro amesema wametia mbaroni Hadija Omar mkazi wa ukonga kwa kuwahifadhi wasichana 15 walio chini ya umri wa miaka 16 ambao walitaka kuwasafirisha kwenda oman kinyume cha sheria.
Akizungumzia zoezi la uhakiki wa silaha Cp Siro amesema hadi sasa silaha 3,099 zimehakikiwa na kutangaza kuwa zoezi hilo litafungwa rasmi tareh 30 baada ya hapo Operesheni kubwa ya kutafuta sihala hizo itaanza.
No comments:
Post a Comment