Monday 16 May 2016

Mwenge wa uhuru umewasili jijini Dar es salaam na haya.


Mwenge wa Uhuru Umewasili leo katika jiji la dsm ukitokea katika mkoa wa mjini Magharibi Visiwani Zanzibar ambapo umepokelewa na mkuu wa mkoa wa dsm Paul Makonda na kutarajia kuzindua miradi na uwekaji wa jiwe la msingi miradi 22 yenye thamani ya shilingi billion 19 katika wilaya za Kinondoni,Ilala na Temeke.

Katika Uwanja wa ndege Mwenge huo uliwasili majira ya saa mbili asubuhi aambapo awali ulikabidhiwa kwa katibu tawala wa Mkoa wa dsm Teresia Mbando kabla ya kukabidhiwa mkuu wa mkoa wa dsm na baadae kukabidhi kwa Mkuu wa wilaya ya kinondoni kuanza kutembelea na kuzindua miradi mbali mbali.

Mkuu wa Mkoa wa dsm Paul makonda akizungumza mara baada ya kupokea mwenge huo amesema lengo la mwenge wa Uhuru ni kupinga vitendo vya uonevu,Rushwa ,dhulma kwa wanyonge kupiga vita maradhi ikiwemo maambikizi ya Ugonjwa wa Ukimwi,Unyanyapaa pamoja na kueneza upendo na kupinga vitendo vyote vya ukandamizaji dhidi ya wanyonge.

Aidha amesema kauli mbiu ya mwaka huu Vijana ni nguvu ya kazi ya Taifa washirikishwe na kuwezeshwa inalenga kuwasaidia Vijana katika kuhakikisha wanafanya Shughuli za kiuchumi na kimaendeleo huku serikali ikiweka mazingira wezeshi.

Viongozi mbali mbali kutoka manispaa za mkoa wa dsm kutoka vyama mbali mbali vya kisiasa walihudhuria mapokezi hayo ambapo pia wakishiriki katika uzinduzi wa mradi wa soko la kisasa lililopo mburahati ambalo linajengwa kwa njia ya Ubia katika ya Danida pamoja na halmashauri ya manispaa ya Kinondoni mradi ambao utagharimu kiasi cha Shilingi Billion moja.

No comments:

Post a Comment