Wednesday 11 May 2016

Rais Dk.John Magufuli aondoka nchini kwenda Uganda kuungana na Museveni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameondoka nchini leo majira ya saa nne asubuhi kuelekea Uganda akitokea jijini Arusha.

Rais Magufuli ataungana na viongozi wengine hapo kesho tarehe 12.05.2016 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ambaye alishinda katika uchaguzi mkuu wa wa mwezi Februari 2016.

Wakati akielekea katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA Rais Magufuli amesindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiq pamoja na Mkuu wa Mkoa wa ArushaFelix Ntibenda.

Rais wa Uganda ataapishwa kesho kuongoza taifa hilo baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa taifa hilo mwezi Februari kwa asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa.

Wakati huo viongozi wa chama cha upinzani cha FDC walitangaza kufanya maandamano kuzuia kuapishwa kwa Rais Museveni maandamano ambayo yalinyimwa kibali na wanajeshi kutanda jiji la Kampala.

No comments:

Post a Comment