Tuesday 17 May 2016

Taarifa kamili ya David Kafulila kushindwa kesi hii hapa.


Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ameshindwa katika kesi aliyoifungua kupinga ushindi wa Hasna Mwilima wa CCM.
Kesi ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora na ilikuwa chini ya Jaji Ferdinand Wambari.
Katika kesi hii upande wa mlalamikaji (Kafulila) uliongozwa na mawakili Prof. Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Lumenyera, Ili hali upande wa mlalamikiwa (Husna) uliongozwa na wakili Kennedy Fungamtama pamoja na Mawakili wa Serikali upande wa mwanasheria mkuu wa Serikali.

No comments:

Post a Comment