Kufuatia Kushuka kwa Ufaulu kwa masomo ya Kiingereza,Sayansi na Hisabati katika Wilaya za Nachingwea na Ruangwa Mkoani Lindi Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) kwa kushirikiana na
Wizara ya Elimu,Sayansi,na Teknolojia,Pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imewezesha awamu ya pili ya Programu ya kujenga uwezo wa walimu na wanafunzi,kwa walimu mahiri (Msingi) wa masomo ya Hisabati, Kiswahili na Kiingereza wilayani Ruangwa.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha walimu kuwatambua wanafunzi wenye uwezo mdogo kimasomo na kuwapatia mafunzo rekebishi na kuwajengea uwezo ili wote wawe na uelewa unaolingana.
Akiongea na Waandishi wa Habari Leo Wilayani Ruangwa Afisa Mahusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Elimu(TEA) Makao Makuu,Bw Tito Nghanwa ameeleza kuwa Programu ya kujenga uwezo wa walimu na wanafunzi katika ufundishaji na ujifunzaji ni moja kati ya mikakati 9 iliyoibuliwa katika sekta ya elimu ambao unatekelezwa kupitia mafunzo kwa walimu, na kufadhiliwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania.
Afisa Elimu Taaluma Wilaya ya Ruangwa Mwalimu Lulu Nchia Alikiri Kuwepo kwa Changamoto ya Uwiano wa Walimu na Kubainisha Jitihada Zilizoanzwa Kufanywa na Ofisi ya Elimu ya Wilaya Hiyo
Baadhi ya Walimu wa Shule za Msingi wanaoshiriki Mafunzo ya Siku Tano kupitia Program ya Mafunzo wezeshi(STEPS)walieleza Baadhi ya Changamoto ikiwemo walimu Kukataa Kufundisha Masomo ya Sayansi,Kiengereza na Hisabati
No comments:
Post a Comment