Wednesday 11 May 2016

Kontena 115 za Sukari Zabainika Bandari Kavu ya Vingunguti.

makonda-
Sakata la Ufichaji wa Sukari kwa wafanyabiashara katika jiji la dar es salaam limeendelea kuchukua sura mpya baada ya kamati ya ulinzi na Usalama ya mkoa wa dsm kubaini Kontena 115 zikiwa
zimehifadhiwa katika bandari kavu ya PMM iliyopo vingunguti jijini dsm, huku maelezo ya meneja wa ICD hiyo pamoja na Afisa wa TRA kutoka bandarini yakitofautiana, hali iliyosababisha Mkuu wa mkoa kuchunguza Uingizaji wa Sukari iliyotokea Dubai.

Majira ya Asubuhi Mkuu wa mkoa wa dsm PAUL Makonda akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama walifika eneo hilo kutaka kujua bidhaa zilizopo eneo hilo ambapo taarifa za UChunguzi zilibaini kuwapo kontena 164 huku baadae wakisema kontena 115 ambazo ziliwekwa sehemu mbalimbali na kuwa vigumu kuzifungua ili kubaini kilichopo.

Mkuu wa mkoa aliwaamuru kushusha baadhi ya makontena ili yakaguliwe na kubaini sukari iliyopo kiasi cha tani 2990 ambayo inaonyesha inatoka Brazil , lakini mifuko ikionyeshwa kupakiwa kutoka Dubai, hali ambayo pia iliwapa mashaka kuhusu ubora na kuitaka TFDA pamoja na TBS kuifanyia Uchunguzi.

Baada ya mabishano hayo Makonda aliamuru kufanyika kwa Uchunguzi wa Makontena yote na kuwataka maafisa wa TRA ,Polisi na Takukuru kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakiki bidhaa zilizokuwapo.

Aidha Kamati hiyo ilifanya ukaguzi katika ghara la Mfanyabiashara Mohamed Interprises ililopo vingunguti ambapo ilikutwa sukari nyeupe kiasi cha tani 2500 na kuitaka isiuzwe wala kusambazwa mpaka pale itakapothibitishwa Ubora wake na mamlaka ya chakula na dawa pamoja na TBS, baada ya kubaini kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanauza sukari kwa kuiweka katika mifuko mipya ikiwa imekwisha muda wa matumizi.

No comments:

Post a Comment