Akichangia hotuba ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Zitto amesema kwamba siku walipochangia kauli ya serikali kuhusu bunge kutorushwa live wabunge walio kataa kuunga mkono serikali wameitwa kuhojiwa.
''Mimi nashangaa sana siku Waziri Nape ametoa kauli ya serikali kuhusu kurushwa kwa matangazo ya Bunge wabunge tulichangia wapo waliounga mkono na wengine tukakataa kuunga mkono''- Amesema Zitto.
''Mheshimiwa Naibu Spika kiti chako kimetuita wabunge wote tuliopinga kauli ya Waziri Nape kwenye kamati ya maadili mimi jana nimepata barua kwamba mnatubana kusema mnazuia bunge lisionekane hata kutoa maoni ndani ya bunge mnatuita kwenda kuhojiwa, mnaturudisha nyuma namna hii? Amehoji Zitto.
Aidha Zitto ameonyesha pia kutoridhika na vyombo vya habari nchini runinga na redio kucheza nyimbo nyingi za wasanii wa nje n kusahau wasanii wa ndani na kuitaka serikali kupitia kwa waziri husika kuchukua hatua.
''Waziri Nape hili lipo kwako kama unataka kuwatetea wasanii hili wala halihiitaji kubadilisha sheria na kanuni za kontenti zipo chini ya waziri. Toa kanuni TCRA wazibariki kuwa asilimia 80 ya nyimbo zitakazopigwa kwenye redio na TV zetu ziwe za wasanii wetu wa Tanzania basi,” amesema Zitto.
No comments:
Post a Comment