Thursday 2 June 2016

Baadhi ya waalimu wakuu wakiuka agizo la Mh.Raisi Magufuli kwa kuhuza madawati kwa mafundi Sofa.

Serikali imejiridhisha kuwepo kwa walimu wakuu wasiowaaminifu ambao wamekua wakiuza madawati kwa mafundi mbao na kuyabadilisha na kutengeneza thamani za bidhaa zitokanazo na mbao ikiwemo masofa jambo ambalo limekua likirudisha nyumba juhudi za serikali katika kuboresha elimu.


Akiongea na wakati wa kukagua maendeleo ya utengenezaji wa madawati ikiwa ni utekerezaji wa agizo la rais jonh pombe magufuli kwa wakuu wa wilaya wote hapa nchini kukamilisha tatizo la madawati kwa wanafunzi, mkuu wa mkoa wa morogoro Stephen Kebwe amesema kumekuwapo kwa walimu wengi ambao sio waaminifu katika kazi zao wamekua wakiuza madawati kwa mafundi wa mbao jambo ambalo alishawai kukutana nalo katika uongozi wake na kuwaagiza wakuu wa wilaya kusimamia madawati hayo ambayo yanatengenezwa sasa.

Mkuu wa mkoa wa morogoro amewaagiza watendaji wa kata na vijiji kufanya kazi za kiofisi mwisho saa nne asubui na baada ya hapo kwenda kusimamia kikamilifu zoezi la utengenezaji wa madawati huku mkuu wa wilaya ya mvomero Elizabeth Mkwasa akiadi kutekereza agizo la rais magufuli la upatikanaji wa madawati yote kwa wanafunzi wa shule ya msingi ifikapo june 30 mwaka huu.



USISAHAU KULIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA,KUTU FOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment